Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, May 31, 2012

Waziri wa zamani wa Rwanda ahukumiwa kwa kuhusika na mauaji ya kimbari

Mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda ICTR imemhukumu Callixte Nzabonimana kifungo cha maisha jela baada ya kumpata na hatia ya kuhusika pakubwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Nzabonimana alikuwa Waziri wa Vijana wakati mauaji hayo yalipotokea. Mahakama ya ICTR imesema ushahidi unaonyesha kuwa Callixte Nzabonimana aliwachochea Wahutu kuwaua Watutsi na vilevile imedaiwa kwamba Waziri huyo wa zamani wa Rwanda alitiliana saini mikataba miwili na waasi wa Interahamwe wa kabila la Hutu ili kufanikisha mauaji ya watu wa kabila la Watusi. Callixte Nzabonimana alikamatwa mwaka 2008 nchini Tanzania. Mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda yalipelekea kuuawa zaidi ya watu laki 8, wengi wao wakiwa wa kabila la Watutsi.

No comments: