Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 22, 2012

Rais wa Yemen asema, ataendeleza mapambano dhidi ya mtandao wa al Qaida

Rais Abdu Rabuh Mansur Hadi wa Yemen amesema kuwa, serikali yake itaendeleza mapambano dhidi ya mtandao wa al Qaida, licha ya mtandao huo kufanya shambulizi kubwa jana mjini Sana'a lililopelekea zaidi ya watu 100 kuuawa na wengine wapatao 300 kujeruhiwa.
Huku hayo yakiripotiwa, televisheni ya al Alam imesema kuwa, idadi ya watu waliouawa kwenye shambulio hilo imeongezeka na kufikia 112 na wengine 300 kujeruhiwa wote wakiwa ni maafisa wa jeshi.
Mtandao wa al Qaida umetangaza kuhusika na shambulio hilo na kusema kuwa ulimkusudia Waziri wa Ulinzi wa Yemen na Mkuu wa Jeshi la nchi hiyio, Ahmad Ali al Ashul.
Kwa upande wake, shirika la habari la Xinhua limemnukuu msemaji mmoja wa mtandao wa al Qaida akiliambia shirika hilo kwamba, mwanamgambo mmoja wa mtandao huo aliyevaa nguo za jeshi alijiunga na paredi ya wanajeshi hao katika Medani ya al Sabeen, mjini Sana'a na kujiripua.

No comments: