Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 22, 2012

Mahmoud az Zahar: Utawala wa Kizayuni unaelekea kusambaratika

Mmoja wa viongozi waandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unaelekea kusambaratika.
Televisheni ya al Alam imemnukuu Bw. Mahmoud az Zahar akisema hayo pambizoni mwa Kongambano la Taifa la Kushikamana na Misingi ya Palestina lililofanyika mjini Ghaza na kuongeza kuwa, Israel haiwezi kukwepa hatima yake ya kusambaratika na kufutika kabisa katika uso wa dunia.
Ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni ni donda ndugu la kensa katika eneo la Mashariki ya Kati na kwamba hivi sasa baada ya kupita miaka 64 ya kupandikizwa kwake, donda ndugu hilo limekaribia kuangamia.
Kongamano la Nne la Taifa la Kushikamana na Misingi ya Palestina lilifanyika jana mjini Ghaza na kuhudhuriwa na mamia ya Wapalestina na wanaharakati wa kigeni wanaopigania haki za taifa madhulumu la Palestina.

No comments: