Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, May 5, 2012

Rais wa Malawi amtaka al Bashir kutoshiriki mkutano wa AU nchini mwake

Rais Joyce Banda wa Malawi ameutaka Umoja wa Afrika kumzuia Rais Omar al Bashir wa Sudan kushiriki katika mkutano wa AU unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai nchini mwake.
Bi. Banda ambaye ameingia uongozini mwezi uliopita amesema kwamba, ameitaka AU kutomwalika al Bashir katika mkutano wa viongozi wa jumuiya hiyo utakaofanyika nchini Malawi mwezi Julai. Hatua hiyo ya Rais mpya wa Malawi inaonekana kuwa ni kwa ajili ya kuvutia misaada ya kigeni iliyosimamishwa kwa nchi hiyo katika kipindi cha rais wa kabla yake.
Rais Omar al Bashir wa Sudan aliitembelea Malawi mwaka uliopita wakati Bingu wa Muatharika alipokuwa madarakani.
Rais Bingu wa Muatharika wa Malawi alifariki dunia mwezi uliopita kutokana na mshituko wa moyo.
Itakumbukwa kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC inadai kwamba, Rais wa Sudan anahusika na jinai za kivita, madai ambayo yamekanushwa vikali na serikali ya Khartoum na kusema ni katika siasa za kindumilakuwili za madola ya kibeberu dhidi ya mataifa huru duniani.

No comments: