Kofi Annan mpatanishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mgogoro wa Syria, amesema kwamba, mpango wa amani nchini humo unaendelea vizuri.
Msemaji wa mpatanishi huyo, Ahmad Fawzi, amemnukuu Kofi Annani akisema hayo jana na kuongeza kwamba, mazungumzo yanafanyika kati ya serikali ya Syria na wapinzani wa nchi hiyo ili kumaliza uadui wote.

![]() |
Kofi Anan - aliyekuwa Katibu mkuu wa UN |
Fawzi aidha amesema, licha ya mazungumzo kuendelea lakini katika baadhi ya maeneo bado kunashuhudiwa ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kwamba mgogoro ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja ni wazi kuwa hauwezi kutatatuliwa kwa siku moja au wiki moja.
Kwa mujibu wa mpango wa amani wenye vipengee sita uliopendekezwa na Kofi Annan nchini Syria, Umoja wa Mataifa utapeleka waangalizi 200 hadi 250 wasio na silaha nchini humo.
Mpango huo pia unayataka magenge yenye silaha yanayopinga serikali ya Syria kuweka silaha chini na kusitisha mapigano nchini

No comments:
Post a Comment