Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, May 20, 2012

Mtuhumiwa wa shambulio la Lockerbie la mwaka 1988 afariki dunia

Abdul Basit al Megrahi, afisa wa kijasusi wa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi anayetuhumiwa kuhusika katika shambulizi dhidi ya ndege ya Pan American kwenye anga ya Lockerbie huko Scotland mwaka 1988 amefariki dunia kutokana na maradhi ya saratani.
Afisa huyo alirejeshwa nchini Libya tarehe 20 Agosti 2009, kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya utawala wa Muammar Gaddafi na Scotland.
Madaktari walisema wakati huo kuwa, kulingana na maradhi yake ya kensa, Megrahi alikuwa na miezi mitatu tu ya kuishi.
Inadaiwa kuwa, Uingereza ilimrejesha nyumbani afisa huyo kama njia ya kuwashawishi viongozi wa wakati huo wa Libya waifungulie London milango zaidi ya kibiashara katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika yenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Khaled al-Megrahi, mwana wa kiume wa afisa huyo amethibitisha kifo cha baba yake kwa njia ya simu lakini amekataa kuhojiwa.
Afisa huyo wa Libya mara zote alikuwa akikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile na shambulio hilo la mwaka 1988 lililopelekea watu 270 kuuawa wengi wao wakiwa ni Wamarekani.

No comments: