Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, May 21, 2012

Harakati ya Hamas: Wazayuni wanataka kuushambulia msikiti wa al-Aqswa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetahadharisha kuwa, walowezi wa Kizayuni wanataka kuushambulia msikiti mtakatifu wa al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu. Chama cha Hamas kimewataka Wapalestina kukusanyika katika msikiti huo mtakatifu ili kuwazuia walowezi hao wa Kizayuni kutoushambulia msikiti huo.
Aidha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeitaka Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC kuwaunga mkono Wapalestina katika njia yao ya istiqama na kusimama kidete dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel umeongeza kasi ya njama zake za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina, ambao lengo lake ni kubadilisha muundo wa kijiografia na kijamii wa Palestina.

No comments: