Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, May 20, 2012

Mshauri ya Kiongozi Muadhamu: Iran haiwezi kuvumilia mashinikizo yoyote yale

Mshauri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Iran haitovumilia mashinikizo yoyote yale na itachukua uamuzi kuhusiana na suala la nishati ya nyuklia bila ya kuathirika na mashinikizo au vitisho. Ali Akbar Velayati amezungumzia mashinikizo tarajiwa wakati huu wa kukaribia duru ijayo ya mazungumzo ya Iran na kundi la 5+1 na kubainisha kwamba, Tehran itafanya mazungumzo yajayo katika fremu ya sheria za kimataifa.
Velayati amesema, kutakuwa na matumaini ya kufikiwa natija katika mazungumzo yajayo ya Iran na 5+1 huko Baghdad endapo tu madola ya magharibi yataonyesha nia njema na kuweka kando utwishaji mambo usio wa kisheria. Inafaa kukumbusha hapa kuwa, duru ijayo ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq.

No comments: