Milipuko ya mabomu isiyopungua miwili jana usiku ilisikika huko Kabul muda mfupi baada ya ziara ya ghafla ya Rais Barack Obama wa Marekani huko Afghanistan. Obama jana usiku aliwasili Afghanistan huku kukiwepo na ulinzi mkali. Mlipuko mmoja uliosababishwa na bomu lililokuwa limetegwa katika gari ulitokea katika eneo la barabara ya Jalalabad, kunakopatikana vituo kadhaa ya wanajeshi vamizi wa kigeni. Hayo yamesemwa mapema leo na Mohammad Ayoub Salang mkuu wa polisi wa Kabul. Rais Obama na mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai wamesaini makubaliano kadhaa yanayohusu masuala ya kijeshi na yasiyo ya kijeshi na hivyo kuimarisha zaidi miaka kumi ya misaada ya Marekani kwa Afghanistan baada ya vikosi vya NATO kundoka nchini humo mwaka 2014. Makubaliano hayo yanajumuisha utoaji misaada na washauri kwa Afghanistan katika kipindi cha miaka kumi baada ya kuondoka vikosi vamizi vya NATO mwaka 2014 . Hadi kufikia sasa hakuna tararifa zozote zilizotolewa kuhusu maafa na hasara zilizosababishwa na milipuko hiyo ya Kabul. Wakati huo huo kundi la Taliban la Afghanistan limedai kuwa milipuko ya Kabul ilikusudiwa kumlenga Rais Obama wa Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment