Jamal Tajuddin mwanachama wa ngazi ya juu wa Ikhwanul Muslimin ya Misri amesema kuwa rais mpya wa nchi hiyo atakuwa shaksia mwenye mielekeo ya Kiislamu. Tajuddin amesema kuwa mbali na uchaguzi, raia wa Misri hivi sasa wanaihitaji uhuru, uadilifu wa kijamii na heshima ya utu kuliko wakati mwingine wowote ule. Amesema Wamisri wanahitaji mgombea ambaye watamuamini katika kutekeleza matarajio yao. Jamal Tajuddin mwanachama wa ngazi ya juu ya kundi la Ikhwanul Muslimin la Misri ameongeza kuwa mafanikio makubwa zaidi ya mapinduzi ya Misri ni hatua ya wananchi kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi wa Rais kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo. Kampeni za uchaguzi wa rais wa Misri zimeanza rasmi tangu tarehe 30 mwezi Aprili kote nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment