Abdulhadi al Khawaja mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahrain ambaye amefungwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa wa nchi hiyo amesema ataendelea na mgomo wake wa kula chakula. Al Khawaja ambaye kwa muda sasa amegoma kula chakula akiwa katika jela za utawala wa Aal Khalifa akilalamikia hukumu iliyotolewa dhidi yake na mahakama moja ya Manama mji mkuu wa Bahrain amesema kuwa ataendelea na mgomo wake huo wa kususia kula aliouanza siku 85 zilizopita.
Mwandishi wa kanali ya televisheni ya BBC ambaye alifanikiwa kuonana na kuzungumza kwa dakika tano tu na Abdulhadi al Khawaja baada ya kufanya juhudi kubwa, ameeleza kuwa hali ya kimwili ya mtetezi huyo wa haki za binadamu wa Bahrain ni mbaya kutokana na kukonda sana. Abdulhadi al Khawaja ambaye ana uraia wa Denmark huku akiwa na asili ya Bahrain mwezi Juni mwaka jana alihukumiwa kwenda jela na mahakama ya kijeshi ya Bahrain kwa tuhuma za kuchochea maandamano dhidi ya utawala wa nchi hiyo wa ukoo wa Aal Khalifa.

No comments:
Post a Comment