Viongozi wa ngazi za juu wa jeshi la Yemen wametangaza kuwa, kufuatia kushadidi mapigano huko kusini mwa nchi hiyo kati ya vikosi vya nchi hiyo na watu wenye silaha wanaosadikiwa kuwa na mafungamano na kundi la Al Qaida, watu wasiopungua 42 wameuawa. Viongozi hao wamesema kuwa, katika mapigano mengine jeshi la nchi hiyo limelazimika kutumia ndege za kivita na makombora mazito huko katika mji wa Abyen ulioko kusini mwa nchi hiyo na kupelekea kuuawa wapiganaji wengine wa kundi la Al Qaida wapatao 30. Aidha habari zinaripoti kuwa, askari 12 wa jeshi la nchi hiyo waliuawa hapo jana katika mapigano na wanamgambo wa kundi la Al Qaida katika mji wa Al Kud na Zinjibar iliyoko katika mkoa wa Abyen. Wakati huo huo ndege za Marekani zisizo na rubani zimeendeleza mashambulizi makali dhidi ya wanamgambo hao wa kundi la Al Qaida katika maeneo kadhaa ya Yemen.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment