Leo ni Jumanne tarehe 30 Mfunguo Tisa Jamaduth Thani mwaka 1433 Hijiria, inayosadifiana na tarehe 22 Mei 2012 Miladia. 

Siku kama ya leo miaka 22 iliyopita, sawa na tarehe 22 Mei 1990, Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Yemen ya Kusini na Kaskazini walitoa taarifa ya pamoja ya kuundwa Jamhuri ya Yemen. Baada ya nchi hizo mbili kuungana, dikteta wa zamani wa nchi hiyo Kanali Ali Abdullah Saleh alichaguliwa kuwa rais wa Yemen. Inafaa kukumbusha kuwa, mnamo mwaka 1914, baada ya kutiwa saini makubaliano kati ya utawala wa Othmaniya na Uingereza, Yemen ya Kusini ilijitenga kutoka Yemen ya Kaskazini.
Siku kama ya leo miaka 127 iliyopita muwafaka na tarehe 22 Mei 1885, alifariki dunia Victor Hugo mwandishi na malenga mashuhuri wa Kifaransa akiwa na umri wa miaka 83.
Hugo alikuwa muungaji mkono mkuu wa mabadiliko kwa maslahi ya matabaka ya wanyonge na masikini nchini humo. Victor Hugo alizaliwa mwaka 1802 na kuingia kwenye uwanja wa kisiasa akiwa na miaka 25 ambapo alifanikiwa kuchaguliwa kuwa mbunge. Lakini ulipofika wakati wa utawala wa Napoleon wa Tatu alijiengua kwenye uwanja wa kisiasa na kubaidishwa kwa muda wa miaka 20 baada ya kupinga siasa za dikteta Napoleon wa Tatu.Siku kama ya leo miaka 127 iliyopita muwafaka na tarehe 22 Mei 1885, alifariki dunia Victor Hugo mwandishi na malenga mashuhuri wa Kifaransa akiwa na umri wa miaka 83.
Na miaka 100 iliyopita katika siku kama ya leo alizaliwa Herbert Charles Brown mwanakemia wa Uingereza. Brown alizaliwa mwaka 1912 mjini London na familia yake ilihamia Marekani kabla hata hajatimia miaka miwili. Alijiunga na chuo kikuu cha Chicago mwaka 1935 na kusomea kozi ya Kemia na kuendelea na masomo hadi alipofanikiwa kuwa mhazili wa chuo kikuu. Mwaka 1979 alitunukia tunzo ya Nobel katika taaluma ya Kemia kutokana na jitihada alizofanya katika ugunduzi wa michanganyiko mipya ya Kemia Kaboni au Organic Chemistry. Herbert Charles Brown alifariki dunia mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment