Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani hatua ya kasisi mmoja wa Marekani ya kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu na kusema kuwa, kitendo hicho kimefanyika katika misingi ya kuendeleza chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya na Marekani.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imesema kuwa, ni jambo lisilo na shaka kwamba kitendo cha kasisi huyo wa Kimarekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu kitazidisha chuki za kidini na kitazusha hasira kubwa za Waislamu kote ulimwenguni.
Terry Jones, kasisi wa Kimarekani mwenye chuki kubwa za kidini, ambaye katika maadhimisho ya Septemba 11 mwaka jana alichoma moto nakala kadhaa za Qur'ani Tukufu, juzi Jumapili tarehe 29 Aprili, alirejea tena kitendo hicho cha kishenzi katika kijikanisa chake kidogo huko Gainesville, Florida.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia imeilaumu serikali ya Rais Barack Obama wa Marekani kwa kushindwa kuzuia kitendo hicho na kusema kuwa hayo ni matokeo ya hatua ya Washington ya kunyamazia kimya kitendo cha kinyama cha wanajeshi wa Marekani cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu katika kambi ya Jeshi la Anga la Marekani huko Bagram Afghanistan.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aidha imeitaka Marekani iuombe radhi mara moja
No comments:
Post a Comment