Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mifumo ya kibepari inawadhulumu, kuwadanganya na kuwatumia vibaya wafanyakazi, lakini Uislamu ni mkweli mbele ya wafanyakazi na kwamba Uislamu unampa heshima kubwa mfanyakazi. Ayatullahil Udhma Khamenei amesema hayo leo mbele ya maelfu ya wafanyakazi alioonana nao wakati huu wa kukaribia Mei Mosi yaani Siku ya Wafanyakazi Duniani na kuongeza kuwa, hatua ya Mtume Muhammad SAW ya kubusu mkono wa mfanyakazi mmoja katika kile kisa mashuhuri, inatoa somo muhimu na lenye thamani kubwa kwa kila mtu na ni uthibitisho wa kutosha wa kwamba Uislamu unaipa heshima kubwa nguvu kazi.
Mkutano huo umefanyika baada ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kukagua kazi za Shirika la Viwanda vya Kuzalisha Madawa la Darupakhsh na kuongeza kuwa, kazi katika maana yake pana yaani inayojumuisha kazi zinazofanywa kwa mikono, mwili, fikra, elimu na uongozi ni mhimili wa maisha, harakati na maendeleo endelevu ya kila jamii na kuzishinda njama za kiuchumi za maadui kunahitajia hima ya wafanyakazi, wawekezaji, wakurugenzi wa sekta mbali mbali za serikali na sekta binafsi na matabaka mbali mbali ya wananchi ambao wanapaswa kutia hima ya kutumia bidhaa za ndani ili kwa njia hiyo waoneshe wazi nia zao za kweli za kukabiliana vilivyo na maadui.
Ayatullahil Udhma Khamenei amesisitiza pia juu ya udharura wa kupewa nafasi - kadiri inavyowezekana - mantiki na misingi ya kifikra ya Uislamu katika mipango na hatua mbali mbali zinazochukuliwa kuhusiana na kazi na jamii ya wafanyakazi nchini na kuitaja rasilimali na nguvu kazi kuwa ni mabawa mawili ya uzalishaji wa taifa na inabidi kazi za uzalishaji wa ndani ziheshimiwe ili kwa njia hiyo suala la uzalishaji wa taifa liweze kupata maana yake halisi.
Vile vile ameashiria tahadhari zake mbali mbali ambazo amekuwa akizitoa kwa miaka kadhaa sasa kuhusu namna maadui walivyolenga njama zao upande wa kuharibu na kuzorotesha uchumi wa Iran na kuongeza kuwa, dalili za njama hiyo kubwa inazidi kuonekana siku baada ya siku, lakini taifa la Iran kama ambavyo kwa azma yake thabiti limeweza kuvuuka vizuizi vyote vya huko nyuma, Inshaallah katika siku za usoni pia litaweza kuvuuka kwa ufakhari mkubwa vizuizi vyote vitakavyojitokeza mbele yake.

![]() |
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akikagua baadhi ya kazi za uzalishaji madawa nchini Iran, Jumapili, Aprili 29, 2012 |
Ayatullahil Udhma Khamenei amesisitiza pia juu ya udharura wa kupewa nafasi - kadiri inavyowezekana - mantiki na misingi ya kifikra ya Uislamu katika mipango na hatua mbali mbali zinazochukuliwa kuhusiana na kazi na jamii ya wafanyakazi nchini na kuitaja rasilimali na nguvu kazi kuwa ni mabawa mawili ya uzalishaji wa taifa na inabidi kazi za uzalishaji wa ndani ziheshimiwe ili kwa njia hiyo suala la uzalishaji wa taifa liweze kupata maana yake halisi.
Vile vile ameashiria tahadhari zake mbali mbali ambazo amekuwa akizitoa kwa miaka kadhaa sasa kuhusu namna maadui walivyolenga njama zao upande wa kuharibu na kuzorotesha uchumi wa Iran na kuongeza kuwa, dalili za njama hiyo kubwa inazidi kuonekana siku baada ya siku, lakini taifa la Iran kama ambavyo kwa azma yake thabiti limeweza kuvuuka vizuizi vyote vya huko nyuma, Inshaallah katika siku za usoni pia litaweza kuvuuka kwa ufakhari mkubwa vizuizi vyote vitakavyojitokeza mbele yake.
No comments:
Post a Comment