Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 1, 2012

Ajali ya feri yaua watu 105 nchini India, 100 hawajulikani walipo

Watu wasiopungua 105 wamethibitishwa kupoteza maisha na wengine 100 hawajulikani walipo baada ya feri iliyokuwa imepakia watu kupindukia, kupasuka katikati na kuzama huko kaskazini mashariki mwa India.
Habari zinasema kuwa, ajali hiyo ilitokea jana Jumatatu baada ya kukumbwa na upepo mkali kwenye Mto Brahamaputra katika jimbo la Assam la kaskazini mashariki mwa India.
Mkuu wa jeshi la polisi la jimbo hilo, J.N. Choudhury amewaambia waandishi wa habari kuwa, feri hiyo ndogo ilikuwa imebeba karibu watu 350 na ilipasuka vipande viwili baada ya kupigwa na dhoruba ya upepo mkali, na kwamba watu 150 wameokolewa wakiwa salama.
Itakumbukwa kuwa mwezi Oktoba mwaka jana pia, karibu watu 80 walipoteza maisha baada ya boti yao kuzama katika jimbo la West Bangal la mashariki mwa India.

No comments: