Mahakama ya jinai nchini Misri imetoa hukumu ya miaka michache tu jela kwa mtuhumiwa aliyeua waandamanaji 18 katika maandamano yaliyopelekea kung'oka madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, dikteta Hosni Mubarak.
Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo nyepesi dhidi ya Muhammad Ibrahim Abdul Muni'm aliyekuwa mkuu wa polisi katika eneo la Zawiya la kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo Cairo.
Inasemekana kuwa, tarehe 28 mwezi Juni mwaka jana, Muhammad Abdul Muni'm alitoa amri iliyopelekea kuuawa waandamanaji wapatao 18 katika harakati zilizouangusha utawala wa uliopita wa kidikteta.
Wakati huo huo afisa wa ngazi za juu wa gazeti la Misrul Jadid linalochapishwa nchini Misri Amru Abdur Rahman amewataka wanamapinduzi nchi hiumo kuungana na kuwa kitu kimoja ili kukabiliana na njama za mabaki ya utawala wa dikteta Hosni Mubarak.
Naye mjumbe wa chama cha Uhuru na Uadilifu nchini Misri ametilia shaka kura alizopata Ahmad Shafiq, aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa dikteta Hosni Mubarak na kusema kuna uwezekano mkubwa zimechakachuliwa kwa manufaa ya Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Misri.

No comments:
Post a Comment