Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 2, 2012

Uganda yawasaidia waasi wenye mfungamano na Sudan Kusini

Uganda inadaiwa kuwapa silaha na chakula waasi wenye mfungamano na Sudan Kusini ambao wanaendesha harakati zao katika ardhi ya Sudan. Uganda inadaiwa kutoa misaada ya silaha, chakula na mafuta kwa waasi hao wanaoendesha harakati zao katika mkoa wa Kordofan Kusini huko kusini mwa Sudan. Ripoti zinaarifu kuwa Uganda hivi karibuni imeitumia serikali ya Sudan Kusini malori 20 ya bidhaa za chakula na mafuta kwa ajili ya waasi hao huko Kordofan Kusini. Tovuti ya habari ya Safari ya Sudan imeinukuu duru ya habari ya kuaminika katika serikali ya Juba na kuripoti kuwa serikali ya Sudan Kusini imekuwa ikituma shehena kubwa ya silaha na chakula kwa makundi yanayobeba silaha katika mikoa ya Kordofan Kusini na Blue Nile ndani ya ardhi ya Sudan.

No comments: