Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, May 15, 2012

Asilimia 40 ya Wamisri hawajaamua wampigie nani kura

Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa asilimia 40 ya Wamisri hadi hivi sasa hawajaamua wampigie nani kura katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu wa Mei.

Hivi sasa Amr Musa anaongoza katika kura ya maoni akiwa na asilimia 18 akifuatiwa kwa karibu na Abdel Mon'im Aboul Fotouh aliye na asilimia 16.
Wananchi wa Misri wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa kwanza huru wa rais tarehe 23 na 24 mwezi huu wa Mei ambapo duru ya pili ya uchaguzi huo itafanyika tarehe 16 na 17 Juni mwaka huu, kama italazimu.
Uchaguzi huo wa kihistoria utakuwa wa kwanza wa rais, tangu wananchi wa Misri walipompindua dikteta Hosni Mubarak, mwaka 2011, ambaye alikuwa kibaraka mkubwa wa Marekani na adui wa wananchi wa Palestina.

No comments: