Mahakama moja ya Jinai za Kivita nchini Malaysia imempata na hatia ya kutenda jinai za kivita rais wa zamani wa Marekani George W. Bush.
Mahakama ya Jinai za Kivita ya Kuala Lumpur katika kikao cha pili imesema Bush na maafisa kadhaa wa utawala wake walitenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binaadamu. Mahakama hiyo, ambayo ni ubunifu wa waziri mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohammad, katika uamuzi wa kauli moja imesema Bush na washirika wake wakuu akiwemo makamu wa rais wa zamani Dick Cheney na waziri wa zamani wa ulinzi Donald Rumsfeld wana hatia ya kuhusika na utesaji na jinai za kivita. Waziri Mkuu wa Zamani wa Malaysia Mahatir Mohammad amesema ana azma ya kuhakikisha Bush na washirika wake wanatiwa nguvuni. Mahakama hiyo imetajwa kuwa nembo ya hasira za walimwengu kuhusu jinai zinazotendwa na watawala wa nchi za Magharibi ambao kawaida hawachukuliwi hatua na mahakama rasmi za kimataifa.
Katika kikao chake cha kwanza Novemba mwaka jana Mahakama ya Jinai za Kivita nchini Malaysia iliwapata na hatia Bush na Tony Blair Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ya kutenda jinai katika vita vya Iraq.
No comments:
Post a Comment