Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, April 24, 2012

Ziara ya kanisa yageuka msiba Naivasha

Ziara ya kanisa katika mbuga ya wanyama ya Hells Gate, Naivasha, nchini Kenya, siku ya Jumapili, na iliyowashirikisha vijana 53, iliishia kuwa msiba, wakati 7 kati yao walisombwa na maji kufuatia mvua kubwa.
Walikuwa ni kati ya vijana kutoka kanisa la Mukara PCEA, Dagoretti, mjini Nairobi.

Kundi hilo lilikuwa limesafiri kuelekea Naivasha asubuhi, na lilitazamiwa kurudi mjini Nairobi siku hiyo ya Jumapili, mwendo wa saa kumi, kulingana na mchungaji wa kanisa hilo, Nancy Muthoni. 

No comments: