Habari ya mafanikio ya wataalamu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (sepah) nchini Iran ya kutanzua alama za siri za ndege ya kijasusi ya kisasa kabisa ya Marekani isiyokuwa na rubani aina ya RQ170 na kuanza kutengenezwa ndege za aina hiyo hapa nchini imezusha gumzo kubwa katika vyombo mashuhuri vya habari duniani.
Kamanda wa kikosi cha Jeshi la Anga la Iran Meja Jenerali Amir Ali Hajizadeh Jumapili ya jana alitangaza habari mpya zilizopatikana baada ya kutanzuliwa alama za siri za ndege hiyo ya kijasusu ya Marekani iliyokamatwa na wanaanga wa Iran ka kutumia teknolojia ya kisasa.
Kanali ya televisheni ya Russia Today imerusha hewani mahojiano ya Meja Jenerali Ami Ali Hajizadeh akiwaambia Wamarekani kwamba wataalamu wa Iran wamepata siri zote zilizotumiwa kutengeneza ndege hiyo. Televisheni ya Russia Today imetangaza bahari hiyo baada ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon kutangaza kwamba usalama wa ndege hiyo ya RQ170 utawazuia wahandisi wa Kiirani kuelewa teknolojia iliyotumiwa katika kuitengeneza.
Gazeti la utawala ghasibu wa Israel la Jerusalem Post pia limeakisi habari hiyo ya mafanikio ya wataalamu wa Jeshi la Anga la Iran na kusisitiza kuwa utengenezaji wa ndege kama hiyo nchini Iran unafanyika kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana baada ya kutanzuliwa alama za siri za ndege hiyo. Gazeti hilo pia limeashiria kuwa baadhi ya nchi zimeomba Iran izipe teknolojia ya kutengeneza ndege hiyo ya kijasusi ya Marekani na kuandika kuwa Russia na China ni miongoni mwa nchi hizo.
Gazeti la Jerusalem Post limeendelea kuandika kuwa ndege ya kijasusi isiyokuwa na rubani ya RQ170 ya Marekani imekuwa ikitumiwa mno katika operesheni mbalimbali huko Afghanistan na Pakistan tangu mwaka 2010 na wataalamu wa mambo wanasema kuwa imekuwa na mchango mkubwa katika operesheni ya kugunduliwa na kuuawa kiongozi wa zamani wa kundi la al Qaida Usama bin Laden.
Kanali ya televisheni ya Fox News ya Marekani na gazeti la The Guardia la Uingereza pia vimezungumzia maudhui hiyo na kuakisi jinsi wataalamu wa Iran walivyofanikiwa kutengua kitendawili na alama za siri zilizotumika katika kutengeneza ndege hiyo ya kisasa ya ujasusi ya Marekani.
Ndege isiyokuwa na rubani ya kijasusi ya Marekani ilidhibitiwa ikiwa angani na wataalamu wa kikosi cha vita vya kielektroniki wa kikosi cha Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tarehe 4 Disemba mwaka uliopita na kukabidhiwa kwa vyombo husika hapa nchini bila ya kupata madhara. Ndege hiyo ni ya kisasa kabisa ya jeshi la Marekani ambayo utengenzaji wake unafanana na ule wa ndege za kivita zisizogundulika kwa rada na ilianza kutumiwa rasmi na jeshi la Marekani mwaka 2009.

No comments:
Post a Comment