Chama cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuwa, kiini cha hali ya nchi kuwa tete kimetokana na tabia ya Rais Jakaya Kikwete kukumbatia watendaji wabovu. Hayo yameelezwa na Dakta Wilbroad Slaaa Katibu Mkuu wa Chadema ambaye amesisitiza kwamba, watachukua maamuzi magumu yatakayoitikisa nchi, ikiwa ni pamoja na kuongoza maandamano mazito na makubwa ya umma kwa ajili ya kushinikiza mabadiliko ya utawala. Dakta Slaa amesisitiza kwamba, chanzo cha matatizo yanayolikumba taifa ni tabia ya kuwakumbatia watu waovu badala ya kuwachukulia hatua za kisheria na kiutawala. Hayo yanajiri katika hali ambayo, baadhi ya mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu wameanza kuhaha wakijaribu kujinasua; huku Wabunge wakifanya harakati za kuwasilisha hoja Bungeni ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment