Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametabiri kuwa, mchakato wa kufanikisha nukta za pamoja katika mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 katika kikao cha Baghdad utakuwa wa mafanikio zaidi kulinganisha na mazungumzo yaliyofanyika huko Istanbul, Uturuki.
Dk. Ali Akbar Salehi amesema hayo mbele ya waandishi wa habari aliyofanya kwa pamoja na Waziri mwenzake wa Armenia hapa Tehran na kuelezea matumaini yake kwamba hatua kubwa zitapigwa katika kikao kijacho cha kundi la 5+1 na Iran kilichopangwa kufanyika tarehe 23 mwezi ujao wa Mei huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia ameashiria mazungumzo yaliyofana ya Istanbul na kuelezea matarajio yake ya kufikiwa nukta za pamoja za kudumu kati ya pande mbili hizo.
Dk. Salehi amesisitiza pia kuwa masuala yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho cha Baghdad yatatayarishwa kwanza na maafisa husika kabla ya kuanza kufanyika kikao hicho.

No comments:
Post a Comment