Mkuu wa Baraza la Taifa la Mpito la Libya NTC amewataka raia wote wa nchi hiyo kuungana na kuwa kitu kimoja na kushirikiana na baraza hilo na serikali ya mpito ya nchi yao ili kufanikisha mapatano ya kitaifa nchini humo.
Mustafa Abdul Jalil pia amesema, taasisi za kiraia, za wanamapinduzi na matabaka yote ya wananchi wa ya Libya yanapaswa kushikamana na kushirikiana na baraza la NTC na serikali ya mpito ya nchi hiyo ili kuvuuka salama katika kipindi hiki kigumu kinachoikabili Libya hivi sasa.
Abdul Jalil amesisitiza pia kuwa, baraza hilo la taifa la mpito na serikali zinafanya kazi kwa pamoja na zinafuatilia malengo ya pamoja kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama na kufanikisha uchaguzi wa taifa huko Libya.
Kuhusu suala la wanamapinduzi wa Libya, Mkuu wa Baraza la Taifa la Mpito la nchi hiyo amesema kuwa, serikali inafanya juhudi za kuwapatia wanamapinduzi hao, ajira jeshini na pia kwenye taasisi mbalimbali za usalama na za kiraia.

No comments:
Post a Comment