Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 29, 2012

Hali ya hatari yatangazwa katika maeneo ya mpakani ya Sudan

Duru za habari za serikali ya Sudan zimeripoti kuwa hali ya hatari imetangazwa katika maeneo ya mpakani ya nchi hiyo.


Habari zinasema kuwa Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan ametangaza hali ya hatari katika baadhi ya maeneo yenye mpaka wa pamoja na Sudan Kusini.
Hali hiyo ya hatari inayajumuisha baadhi ya maeno ya mkoa wa Kordofan Kusini, Blue Nile na Sinar.
Mivutano iliyojitokeza hivi karibuni kati ya Sudan na Sudan Kusini baada ya Sudan Kusini kuvamia na kukalia kwa mabavu eneo la kusini mwa Sudan imezidisha wasiwasi wa kimataifa juu ya uwezekano wa kuzuka vita kati ya nchi mbili hizo.
Huku Khartoum ikichukua hatua hiyo, Juba imeutaarifu Umoja wa Mataifa kwamba itaondoa polisi wake wote katika maeneo ya Sudan unayoyakalia kwa mabavu na kueleza kuwa imedhamiria kwa dhati kusimamisha mapigano yote na jirani yake Sudan.
 

No comments: