Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kukumbuka tarehe 29 Aprili, siku ya kuwakumbuka wahanga wa silaha za kemikali duniani.
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa unasomeka kama ifuatavyo: "Siku ya kuwakumbuka wahanga wa silaha za kemikali ni siku ambayo inaadhimishwa kwa ajili ya kukumbuka mateso na masaibu yaliyowapata wahanga hao kutokana na silaha hizo zilizo dhidi ya ubinaadamu na haja ya kuangaliwa upya maamuzi yanayochukuliwa kwa lengo la kutokomeza na kupiga marufuku silaha za kemikali duniani kote."
Aidha Ban Ki-moon ameashiria katika ujumbe wake huo kuhusu kutimia miaka 15 ya kutekelezwa makubaliano ya kupambana na silaha za kemikali (CWC) na kuzitolea mwito serikali nane ambazo bado hazijajiunga na mkataba huo kujiunga haraka iwezekanavyo na makubaliano hayo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, hakuna sababu yoyote ya kuyafanya mataifa ya dunia yachelewe kuiokoa dunia kutokana na hatari ya kuweko silaha hizo angamizi zinazosababisha maafa makubwa.

No comments:
Post a Comment