Viongozi wa Saudi Arabia wamezuia kuonyeshwa vitabu vya Harakati ya
Ikhwaanul Muslimiin katika maonyesho ya vitabu mjini Riyadh. Hayo
yamesemwa na Ahmad al-Hamdan, mkuu wa jumuiya ya uchapishaji na
usambazaji vitabu ya Saudia, katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya
mwaka 2014 yaliyofunguliwa leo na kuongeza kuwa, kuonyeshwa vitabu vya
harakati hiyo katika maonyesho hayo ni hatari kwa usalama wa fikra za
kijamii.
Itakumbukwa kuwa siku ya Jumamosi iliyopita, Saudia ilitangaza
kuwa, imezuia ushiriki wa jumuiya 350 za uchapishaji na usambazaji
vitabu katika nchi za Kiarabu na za kigeni, kutokana na jumuiya hizo
kutokuwa na vitabu vinavyoendana na viwango vinavyotakiwa nchini Saudia.
Tarehe 7 mwezi Machi mwaka huu, Saudia iliiweka Harakati ya Ikhwaanul
Muslimiin katika orodha ya makundi ya kigaidi. Hatua hiyo ilichukuliwa
baada ya uungaji mkono wa moja kwa moja wa watawala wa kifalme wa nchi
hiyo kwa jeshi lililoongoza mapinduzi dhidi ya Muhammad Mursi wa Misri,
rais aliyepinduliwa na jeshi la nchi hiyo. Kabla ya hapo pia na katika
kulalamikia uungaji mkono wa Qatar kwa kundi hilo la Ikhwaanul Muslimiin
la nchini Misri, tarehe tano mwezi Machi mwaka huu, Saudia, Imarati na
Bahrain ziliondoa mabalozi wao mjini Doha, suala ambalo lilitajwa kuwa
ni sawa na kutia pilipili kwenye kidonda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment