Serikali ya Nigeria imepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika
Abuja, mji mkuu wa nchi hiyo kwa lengo la kulalamikia kitendo cha
kutekwa nyara wanafunzi wasichana zaidi ya 250 wanaoshikiliwa na kundi
la Boko Haram. Taarifa iliyotolewa na polisi imeeleza kuwa, maandamano
hayo yamepigwa marufuku kutokana na sababu za kiusalama. Taasisi
zilizoratibu maandamano hayo zimeeleza kuwa, zimeshangazwa na uamuzi wa
serikali wa kupiga marufuku maandamano hayo, kwa dhana kwamba
yatafanyika kwa malengo ya kisiasa.
Hayo yanajiri katika hali ambayo,
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimeliweka kundi la Boko Haram kwenye
orodha ya makundi ya kigaidi. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wanafunzi
hao wa shule ya wasichana ya bweni ya Chibok iliyoko katika jimbo la
Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria walitekwa nyara na wanamgambo wa
Boko Haram tokea mwezi Aprili, na hadi leo bado wanaendelea kushikiliwa
na kundi hilo, licha ya kufanyika juhudi za kitaifa na kimataifa za
kutaka kuwakomboa wanafunzi hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment