Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu wa Iran yaani Bunge amesema
kuwa, kuandaliwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kila mwaka
mjini Tehran, ni jambo linaloleta nuru na mwanga kwa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran. Akizungumza kwenye sherehe za kumalizika duru ya 31 ya
mashindano hayo hapo jana, Dakta Ali Larijani amesema kuwa usomaji wa
Qur'ani Tukufu una adabu maalumu na kusisitiza kwamba, mwanadamu hawezi
kutasawari kupata saada na ufanisi kwa kusoma Qur'ani Tukufu bila ya
kuchunga adabu hizo.
Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa, Qarii na
msomaji Qur'ani Tukufu pia ana daraja maalumu kwa Mwenyezi Mungu, na
kwamba daraja hilo huzidi kunyanyuliwa zaidi kila anaposoma Kitabu hicho
kitakatifu. Duru ya 31 ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu
ilimalizika jana, na kwa upande wa qiraa mshindi alikuwa Jaafar Fardi
kutoka Iran, na nafasi ya pili hadi ya tano zilishikwa na washiriki
kutoka nchi za Ufilipino, Misri, Tajikistan na Tanzania. Na katika
upande wa hifdhi, nafasi ya kwanza hadi ya tano zilishikwa na
wawakilishi kutoka Iran, Misri, Afghanistan, Indonesia na Niger.
Mashindano ya mwaka huu yaliwashirikisha washiriki 98 kutoka nchi 75
duniani na kusimamiwa na majaji 12 kutoka nchi za Kiislamu wakiwemo
watano kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment