Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametoa msamaha wa masharti kwa kundi
la Boko Haram linalofanya utekaji nyara na mauaji dhidi ya watu wasio na
hatia nchini humo. Amesema wanachama wa kundi hilo watasamehewa tu
iwapo wataamua kuweka chini silaha zao. Huku akiashiria msamaha
uliotolewa na serikali kwa waasi wa kundi la Harakati ya Ukombozi wa
Niger Delta baada ya wao kuamua kuweka chini silaha, msemaji wa serikali
ya Abuja amewataka Boko Haram watumie fursa iliyotolewa na serikali kwa
ajili ya kupata msamaha kama huo.
Kabla ya kupata msamaha, waasi wa
Niger Delta kwa miaka mingi walivuruga amani na usalama wa eneo hilo
tajiri kwa mafuta kwa kuendesha operesheni za uharibifu. Msamaha wa
masharti kwa kundi la Boko Haram umetangazwa ikiwa yamepita masaa
machache tu baada ya Rais Jonathan kutoa amri ya kuanzishwa operesheni
kubwa ya kupambana na kindi hilo la kigaidi. Boko Haram ni kundi ambalo
tokea mwaka 2003 limekuwa likivuruga usalama wa eneo la kaskazini mwa
Nigeria kwa kuendesha shughuli za ghasia, mauji na utekaji nyara. Kundi
hilo ambalo limeiga misimamo na itikadi za kundi la Taliban la nchini
Afghanistan, limekuwa likifuata misimamo mikali na hata kuwakufurisha
kirahisi wapinzani wao. Vitendo haribifu vya kundi hilo vilifikia kilele
mwezi Aprili uliopita kwa kuwateka nyara wanafunzi wa kike zaidi ya 200
katika shule moja ya bweni. Kitendo hicho cha kushtua kiliwashangaza
wengi duniani ambapo vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vilitumia
vibaya na kipropaganda tukio hilo kwa kulitaja kundi hilo la kigaidi
kuwa ni mwakilishi wa watu wa Nigeria na nembo ya Uislamu. Hii ni katika
hali ambayo kundi hilo ambalo linachukiwa nchini Nigeria lina wauasi
wachache mno kati ya Waislamu wapatao milioni 80 wa nchi hiyo.
Wanaigeria wanaamini kwamba kundi hilo lenye misimamo ya kupindukia
mipaka linaharibu jina zuri la Uislamu na kuwafanya watu wasio Waislamu
kuichukia dini hii tukufu. Wajuzi wengi wa mambo wanaamini kwamba kundi
hilo linatokana na njama za kimataifa na kwamba limeundwa na mashirika
ya kijasusi ya nchi za Magharibi kwa lengo la kuharibu jina la Uislamu.
Katika kuthibitisha madai yao, wataalamu hao wanatolea mfano vitendo vya
uhalifu vya kundi hilo vya kuwateka nyara wanafunzi wa kike katika
shule za Nigeria na vitendo kama hivyo vinavyofanywa na makundi ya
Taliban ya Afghanistan na Pakistan. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa
madola ya Magharibi yanaitazama Ngeria kwa jicho la tamaa ya kikoloni
kutokana na kuwa ni mojawapo ya nchi ambazo zina utajiri mkubwa wa
maliasili katika bara la Afrika. Kwa msingi huo yanafanya njama ya
kuzusha migogoro nchini humo ili kuandaa uwanja wa kuingilia masuala ya
ndani ya nchi hiyo kwa maslahi yao yenyewe. Ni kwa kuzingatia ukweli huo
ndipo wakasema kuwa itakuwa vigumu kwa kundi la Boko Haram kukubali
kuweka chini silaha zake na msamaha wa masharti uliotolewa hivi karibuni
na Rais Goodluck Jonathan wa nchi hiyo. Wataalamu wengine wanasema kuwa
kutolewa kwa wakati mmoja amri ya kupambana na Boko Haram na wakati
huohuo pendekezo la msamaha kwao ni ishara ya wazi kwamba serikali
imeshindwa kulidhibiti kundi hilo. Kundi jingine la wajuzi wa mambo ya
Nigeria linadai kuwepo njama ya kuigawa Nigeria katika sehemu mbili kama
ilivyofanyika huko Sudan ambapo nchi hiyo iligawanywa na Wamagharibi
katika sehemu mbili za kaskazini na kusini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment