Majenerali 10 na maafisa wengine watano wa ngazi za juu jeshini nchini
Nigeria, wamepandishwa kizimbani katika mahakama za kijeshi kwa tuhuma
za kuwa na uhusiano na kundi la kitakfiri la Boko Haram ambalo limekuwa
likifanya mashambulizi ya kila mara nchini humo. Gazeti la Leadership la
nchini Nigeria limeandika leo kwamba mbali na maafisa hao, maafisa
wengine wanne wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za uhaini na
kushirikiana na kundi hilo.
Hayo yanajiri wakati ambao, wiki iliyopita
Chris Olukolade, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo alikadhibisha
taarifa ya kusailiwa baadhi ya majenerali wa jeshi kwa tuhuma za
kushirikiana na Boko Haram. Wanasiasa na hata maafisa wa ngazi za juu
jeshini wamekuwa wakiweka bayana kwamba, baadhi ya maafisa wa jeshi
wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na kundi hilo katika kuendesha
operesheni zake za kigaidi. Wakati huo huo familia za wanafunzi wa kike
waliotekwa nyara na kundi hilo, wameitaka serikali ya Nigeria kufanya
mazungumzo yatakayosaidia kuachiliwa huru wasichana hao. Katika upande
mwingine, viongozi wa jimbo la Borno wamesema kuwa, wasichana ambao wiki
iliyopita walifanikiwa kutoroka kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Boko
Haram, wamepelekwa katika shule za Abuja, Lagos na Kaduna ili waendelee
na masomo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment