Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, June 3, 2014

Netanyahu aikosoa EU kuhusiana na Palestina

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ameikosoa vikali misimamo ya Umoja wa Ulaya ya kuunga mkono makubaliano yaliyofikiwa baina ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina 'Hamas' na ile ya Fat-h huko Palestina ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Taarifa zinasema kuwa, Kamati ya Usalama ya Israel jana ilimpa Netanyahu jukumu la kuandaa vikwazo vipya dhidi ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Inafaa kuashiria hapa kuwa, siku ya Jumapili iliyopita, Waziri Mkuu wa Israel alidai kwamba Hamas ni harakati inayotaka utawala wa Israel utokomezwe, na hivyo kuitaka jamii ya kimataifa kutoitambua rasmi serikali itakayoshirikishwa harakati hiyo.
Hii ni katika hali ambayo, mawaziri wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina waliapishwa jana huko Ramallah, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

No comments: