Kwa mara nyingine tena Umoja wa Mataifa umeonya kuhusiana na mgogoro wa
chakula nchini Sudan Kusini. Toby Lanzer, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa
katika masuala ya misaada ya kibinadamu nchini humo amesema kuwa, hadi
kufikia mwishoni mwa mwaka huu mgogoro wa vita unaoendelea Sudan Kusini
utawasababishia janga la njaa zaidi ya thuluthi moja ya wananchi wa nchi
hiyo changa zaidi barani Afrika. Lanzer ameongeza kuwa, kwa mujibu wa
takwimu za Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni moja na laki tano ambao
wako katika hatari ya kuyakimbia makazi yao, watu laki nane na 50 elfu
ambao ni wakimbizi na wengine milioni nne kwa pamoja wanakabiliwa na
tishio la uhaba mkubwa wa chakula.
Lanzer ameyasema hayo nchini Norway
katika kikao cha wafadhili wa kimataifa kwa ajili ya nchi hiyo.
Washiriki wa mkutano huo wameahidi kuchangia dola milioni 600 kwa ajili
ya kukabiliana na ukame Sudan Kusini. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa anayeshughulikia masuala ya misaada ya kibinaadamu Bi. Valerie
Amos amesisitiza kuwa, haifai kucheleweshwa suala hilo na kusubiri
kuharibika zaidi hali ya mambo, bali kuna udharura wa kumalizwa tatizo
hilo haraka iwezekanavyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment