Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi yake
itapigia kura ya turufu azimio la kutaka kushitakiwa Syria katika
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Vitaly Churkin amesema azimio hilo lililopendekezwa na Ufaransa na
ambalo linatarajiwa kupigiwa kura leo, litarudisha nyuma jitihada za
kuutafutia suluhisho la kisiasa mgogoro wa Syria.
Azimio hilo linavituhumu vikosi vya serikali, wanamgambo wanaounga
mkono serikali na waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya Damascus
kufanya mauaji.
Jana mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar al Jaafari
alizitaka nchi za dunia kutounga mkono azimio hilo akisema kuwa, azimio
hilo ni la upendeleo na lengo lake ni kuzuia fursa ya kutatuliwa mgogoro
wa nchi hiyo kwa njia za amani.
No comments:
Post a Comment