Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Friday, May 23, 2014

Jeshi la Syria laendelea kupata ushindi dhidi ya magaidi

Omran al Zoubi, Waziri wa Habari wa Syria amesema kuwa, jeshi la Syria limepata ushindi na mafanikio makubwa katika vita vyake dhidi ya vibaraka wa Marekani na nchi za Kiarabu nchini humo. al-Zoub amesema kuwa, jeshi la Syria kwa uungaji mkono wa wananchi wa nchi hiyo, limeweza kuwashinda vibaraka hao na kwamba, litaendelea kupata ushindi huo daima. Amesema kuwa, Syria kwa uungaji mkoni wa marafiki wake zikiwemo Russia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, itaweza kurekebisha na kurejesha hali ya mambo nchini humo.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba,  magaidi kutoka zaidi ya nchi 80 za dunia na kwa uungaji mkono wa kifedha na silaha wa madola mbalimbali ya Kiarabu na Ulaya na Marekani, wamekuwa wakipigana vita vikali tangu mwezi Machi mwaka 2011 dhidi ya Syria, ambapo hata hivyo wameshindwa vibaya na jeshi la nchi hiyo katika siku za hivi karibuni. Ni kutokana na mafanikio hayo, ndipo Ufaransa ikaamua kuandaa rasimu ya azimio kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Syria ikidai kuwa nchi hiyo imetenda jinai za kivita. Hata hivyo rasimu ya azimio hilo imepingwa kwa kura ya veto na Russia na China ambazo ni nchi mbili kati ya tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

No comments: