Hit single ya ‘happy’ ya Pharrell Williams ni single ambayo
ukiangalia kwenye mtandao watu wengi walitengeneza video zao na kuziweka
humo lakini kwa kutumia wimbo huohuo ambao kiukweli wanasema ni wimbo
uliovunja rekodi kwenye nchi ambazo hata hakuwahi kuifikia hiyo rekodi.
Kama ilivyotokea kwa mataifa mengine, mashabiki sita wa Pharrell
nchini Iran waliamua kutengeneza video yao wakiwa ni wasichana na
wavulana na baada ya kuirekodi wakaiweka kwenye mtandao.
Iran ikiwa ni nchi ambayo ina sheria zake kazi ikiwemo za dini
zinazobana, iliwachukulia hatua kwa kuwakamata wote sita walioonekana
kwenye video hiyo ambapo mkuu wa Polisi Tehran Hossein Sajedinia
alithibitisha hilo na kwamba baada ya video kusambaa walianzisha
uchunguzi uliofanikishwa watu hao sita kukamatwa baada ya saa sita.
Mkuu huyu wa Polisi amewaonya vijana wa Iran kwamba yeyote
atakaekwenda kinyume na taratibu au kanuni za nchi na dini atakamatwa
kama ilivyotokea ambapo CNN walisema moja ya makosa yaliyofanya watu hao
kukamatwa wakiwemo wasichana ni kucheza kwa kushikana na pia kuacha
wazi nywele na sehemu nyingine za mwili.
Baada ya watu hawa kukamatwa walikiri kwamba haikua lengo lao kuiweka
hiyo video online ambapo mwingine alisema walitokea kwenye video ikiwa
ni sehemu ya mazoezi ya kuigiza kwenye TV.
Baada ya kukamatwa kwa watu hao sita Mwandishi wa habari wa Iran
Golnaz Esfandiari aliandika ‘Iran ni sehemu ambayo ukiwa na furaha
unakamatwa’
Hata hivyo taarifa za saa kadhaa zilizopita zinasema watu hawa
inaaminika wameachiwa kwa dhamana baada ya kuchukua headlines iliyoanzia
kwenye kituo cha taifa cha TV ambapo walihojiwa camera zikichukua picha
kutoka migongoni mwao, yaani hawakuonekana sura.
Mmoja wa sita hao walikua wameshikiliwa aitwae Taravati
alipost kwenye Instagram na kummention Pharrell kwa kusema ‘hI,
nimerudi… asante sana Pharrell na kila mmoja alietujali nawapenda wote
sana na niliwamiss’
No comments:
Post a Comment