Wapiganaji kadhaa wa kundi la Boko Haram wameuawa kufuatia
mashambulio ya anga na ardhini ya jeshi la Nigeria kaskazini mashariki
mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Kanali Muhammed Dole, msemaji wa
divisheni ya 7 ya jeshi la Nigeria mjini Maiduguri amewaambia wana
habari kwamba, idadi kubwa ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko
Haram wameuawa baada ya kambi zao za siri kushambuliwa magharibi mwa mji
wa Maiduguri.
Mashambulio ya jeshi la Nigeria yanatekelezwa baada ya
kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau kukiri hivi karibuni kwamba,
kundi lake ndilo lililohusika na shambulio dhidi ya kambi moja ya
kijeshi katika mji wa Maiduguri.
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria mwezi Mei mwaka huu alitangaza hali
ya hatari katika majimbo ya Yoba, Borno na Adamawa kaskazini mwa nchi
hiyo na kuliamuru jeshi kutekeleza operesheni za kuwasaka wanamgambo wa
Boko Haram katika eneo hilo. Kundi la Boko Haram limetangaza kuhusika
na mashambulio mbalimbali ya umwagaji wa damu katika maeneo tofauti ya
Nigeria tangu mwaka 2009.
No comments:
Post a Comment