Kwa akali watu 16 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa, baada ya
waandamanaji wanaomuunga mkono Muhammad Morsi rais aliyeondolewa
madarakani nchini Misri kupambana na askari wa usalama wa nchi hiyo.
Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin imetangaza kuwa, wafuasi hao wa Mosri
wameuawa mapema leo wakati walipokuwa wakifanya maandamano ya kupinga
kuondolewa madarakani Muhammad Morsi.
Ahmad Aref Msemaji wa Ikhwanul
Muslimiin amesema kuwa, wafuasi hao wa Morsi wameuawa baada ya
kufyatuliwa risasi na askari wa usalama na mamia ya wengine kujeruhiwa,
baadhi yao hali zao zimeripoti kuwa mahututi. Wakati huohuo, Muhammad
Morsi rais aliyondolewa madarakani pamoja na viongozi wengine wanane wa
ngazi za juu wa Ikhwanul Muslimiin wataanza kuhojiwa leo kwa tuhuma za
kuvivunjia heshima vyombo vya sheria vya nchi hiyo. Shakhsia hao pia
wamepigwa marufuku kufanya safari nje ya nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment