Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu wa Zimbabwe amemkosoa vikali Rais Robert
Mugabe wa nchi hiyo kwa kushindwa kutekeleza marekebisho ya kidemokrasia
nchini humo. Akihutubia kwenye mkutano wa kampeni, Tsvangirai ambaye
pia ni kiongozi wa chama cha MDC amesema kuwa, inashangaza kuona kwamba
zimeanza kampeni za uchaguzi kabla ya kufanyika marekebisho muhimu ya
demokrasia nchini humo. Waziri Mkuu wa Zimbabwe ambaye ni hasimu mkubwa
wa kisiasa wa Rais Mugabe amesisitiza kuwa, atashiriki kwenye
kinyang'anyiro cha uchaguzi ujao wa rais, ijapokuwa marekebisho hayo
yangesaidia uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Imepangwa kuwa, uchaguzi
wa rais na bunge nchini Zimbabwe utafanyika Julai 31 mwaka huu. Inafaa
kuashiria hapa kuwa, Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC
ilimshinikiza Rais Mugabe na kumtaka aitishe uchaguzi baada ya wiki
mbili tokea tarehe iliyopangwa awali, lakini Mahakama ya Katiba ya nchi
hiyo ilipinga takwa hilo na kusisitiza juu ya kufanyika uchaguzi huo
katika tarehe iliyopangwa awali, yaani Julai 31 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment