Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, July 6, 2013

Wamisri waendelea kuandamana, 6 wauawa

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Misri huku kukiwa na habari za kutokea fujo katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.
Wafuasi wa rais aliyepinduliwa, Muhammad Morsi wameendelea kuandamana kwa siku ya tatu mfululizo wakipinga mapinduzi yaliyofanywa na jeshi siku ya Jumatano dhidi ya kiongozi wao. Mjini Cairo, makumi ya maelfu ya wafuasi wa Dkt. Morsi wamekusanyika katika eneo la Nasr karibu na chuo kikuu cha Cairo huku wakitoa nara za kulaani jeshi la nchi hiyo. Baadhi ya duru zinaarifu kwamba wanajeshi wamewaua watu 6 kwa kuwapiga risasi wakati idadi kubwa ya wafuasi wa Morsi walipokuwa wakiandamana kuelekea kambi ya kijeshi ya Republican Guard.
Hata hivyo, Msemaji wa jeshi amekanusha habari hizo na kusema hakuna mtu aliyeuawa ingawa kuna watu kadhaa ambao wamejeruhiwa. Inaaminika kwamba Dkt. Morsi na maafisa wengine wa ngazi za juu wa Ikhwanul Muslimin wanazuiliwa na jeshi katika kambi hiyo.
Huku hayo yakijiri, rais wa mpito Adly Mansour amelivunja bunge la Seneti na kumteua mkuu mpya wa vyombo vya usalama. Mansour anatarajiwa kutoa tamko hapo kesho kulielezea taifa jinsi anavyopanga kutekeleza ramani ya njia iliyotangazwa na jeshi siku ya Jumatano.

No comments: