Mahakama ya Kilele nchini Zimbabwe imetupilia mbali ombi la Rais
Robert Mugabe la kutaka tarehe ya uchaguzi isogezwe mbele na badala yake
imesisitiza kwamba uchaguzi wa rais lazima ufanyike Julai 31 kama
ilivyoamuliwa huko nyuma.
Jaji Mkuu wa Zimbabwe, Godfrey Chidyausiku amesema mahakama hiyo
haina mamlaka ya kubadilisha uamuzi wake wa huko nyuma. Rasi Mugabe
alikuwa ameomba tarehe hiyo ibadilishwe baada ya kushinikizwa na Jumuiya
ya SADC pamoja na Waziri Mkuu wake, Morgan Tsvangirai.
Chama cha MDC kinachoongozwa na Tsvangirai kimesema uamuzi huo wa
korti unavunja moyo lakini kimesisitiza kwamba, kitaanza kupanga
mikakati ya kujiandaa kwa uchaguzi huo. Msemaji wa Tsvangirai, Luke
Tamborinyoka amesema Waziri Mkuu amekubali kuheshimu maamuzi ya Mahakama
ya Kilele na kwamba kitakachofuata ni kuanza kujiandaa kwa ajili ya
uchaguzi.
No comments:
Post a Comment