Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imesema kuwa idadi ya watu
waliouawa katika mashambulizi ya leo ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya
wafuasi wa Muhammad Morsi, rais wa nchi iyo aliyepinduliwa na jeshi
imeongezeka na kufikia watu 53 wakiwemo watoto watano.
Ikhwanul Muslimin imesema kuwa, wafuasi wake wameuawa wakati jeshi la
Misri lilipoushambulia umati wa watu hao waliokuwa wameketi chini nje
ya kambi zao wakipinga kitendo cha kupinduliwa Rais Muhammad Morsi.
Wizara ya Afya ya Misri imetaja idadi ya waliouawa kwenye
mashambulizi hayo ya jeshi ya leo kuwa watu 40. Watu walioshuhudia
wameeleza kuwa jeshi la Misri limetumia silaha hai kuwatawanya wafuasi
wa Muhammad Morsi huko katika mji wa Nasr mashariki mwa Cairo.
No comments:
Post a Comment