Sheikh Mkuu wa al-Azhar ya Misri, ametoa wito kwa jeshi la nchi
hiyo akilitaka liwaachie huru viongozi waandamizi wa Harakati ya Ikwanul
Muslimin ili kupunguza hasira za wafuasi wa Mohammad Mursi, rais
aliyepinduliwa wiki iliyopita.
Sheikh Ahmed al Tayyib amesema Misri inaelekea pabaya na ametaka
juhudi zifanywe ili kuanza mara moja maridhiano ya kitaifa. Dkt Muhammad
Morsi na wenzake wanaendelea kushikiliwa katika kambi ya kijeshi ya
Republican Guard mjini Cairo.
Huku hayo yakijiri, Ikhwanul Muslimin imewataka wafuasi wake
kupambana na jeshi la nchi hiyo ili kulinda demokrasia. Hii ni baada ya
jeshi kuwafyatulia risasi wafuasi wa Dkt. Mursi na kuua zaidi ya 40 kati
yao. Jeshi limelazimika kufanya mkutano na waandishi wa habari na
kusema wafuasi wa Ikhwani ndio wa kulaumiwa kutokana na mauaji
yaliyotokea.
Wakati huohuo nchi mbalimbali zimelitaka jeshi la Misri likomeshe
mauaji dhidi ya wafuasi wa Mohammad Morsi. Umoja wa Mataifa pia
umeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya mambo nchini Misri. Katibu Mkuu
wa UN, Ban Ki-moon amesema hali ya Misri inatia wasiwasi na ametaka
hatua za haraka zichukuliwa kulinda maisha ya raia.
No comments:
Post a Comment