Rais wa serikali ya mpito ya Misri Adly Mansour ametangaza kwamba uchaguzi wa bunge nchini humo utafanyika mwaka 2014.
Rais Mansour ameongeza kuwa, mara baada ya kufanyika uchaguzi wa
bunge, itatangazwa tarehe ya kufanyika uchaguzi wa rais. Rais wa
serikali ya mpito ya Misri ana kipindi cha miezi sita cha kuifanyia
marekebisho katiba ya nchi hiyo ambayo hivi sasa imesitishwa.
Wakati huohuo, Msemaji wa Rais wa serikali ya mpito wa Misri amesema
kuwa, matukio yaliyojiri jana mjini Cairo hayawezi kuzuia uundwaji wa
serikali mpya. Ahmad al Musalmani amesema kuwa, mapigano yaliyotokea
jana kati ya wafuasi wa Harakati ya Ikhwanul Muslimiin na vikosi vya
usalama mbele ya makao ya Gadi ya Rais mashariki mwa Cairo, hayawezi
kuzuia juhudi za kuundwa serikali mpya au kutekelezwa mpango wa ramani
ya njia uliobuniwa na jeshi la nchi hiyo. Zaidi ya watu 50 waliuawa
kwenye mapigano ya jana na mamia ya wengine kujeruhiwa.
No comments:
Post a Comment