Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umelaani shambulio la
kundi la Boko Haram dhidi ya shule moja ya bweni nchini Nigeria. Taarifa
ya UNICEF imebainisha kwamba, shambulio hilo lililosababisha wanafunzi
28 na mwalimu mmoja kuuawa kinyama baada ya shule yao kuchomwa moto ni
jinai ya wazi hivyo waliotenda jinai ni lazima wafuatiliwe kisheria.
Aidha jana Umoja wa Ulaya nao ulilaani vikali mauaji ya kikatili
dhidi ya wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari ya bweni nchini Nigeria.
Bi Catherine Ashton, Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya sambamba na
kulaani mauaji hayo alitaka magaidi waliofanya jinai hiyo kufuatiliwa
kisheria. Viongozi wa Nigeria wametangaza kwamba, waliohusika na jinai
hiyo watafikiwa na mkono wa sheria.
Wakati huo huo, viongozi wa Nigeria wametangaza kufungwa shule za
sekondari katika jimbo la Yobe kufuatia mauaji ya wanafunzi wa shule ya
msingi yaliyofanywa siku ya Jumamosi.
No comments:
Post a Comment