Umoja wa Mataifa umelaani mauaji yaliyofanywa na jeshi la Misri
dhidi ya waandamanaji nchini humo na kusema kuwa, hali inayotawala
nchini humo inatia wasi wasi. Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa amelaani mauaji dhidi ya waandamanaji wa nchini Misri na
kuyataka makundi yote ya kisiasa katika nchi hiyo kufanya kila yawezalo
kuzuia kuzidi kuharibika hali ya mambo katika nchi hiyo.
Aidha Umoja wa Mataifa umetaka kufanyike uchunguzi huru na kushtakiwa
wale wote waliohusika na mauaji hayo. Taarifa ya Umoja wa Mataifa
imeeleza wasi wasi wake pia kuhusiana na kutiwa mbaroni wanasiasa wengi
nchini humo.
Ban Ki moon amewataka Wamisri kuandamana kwa amani na amelitaka jeshi
la nchi hiyo liache kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji hao. Harakati
ya Ikhwanul Muslimin ya Misri imesema kuwa idadi ya watu waliouawa
katika mashambulizi ya jana ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya wafuasi wa
Muhammad Mursi, imeongezeka na kufikia watu 53 wakiwemo watoto watano.
Ikhwanul Muslimin imesema kuwa, wafuasi wake wameuawa wakati jeshi la
Misri lilipoushambulia umati wa watu hao waliokuwa wameketi chini nje
ya kambi za wanajeshi hao kupinga kupinduliwa Rais Muhammad Mursi.
No comments:
Post a Comment