Umoja wa Ulaya umelaani vikali mauaji ya kikatili dhidi ya
wanafunzi wa shule moja ya sekondari ya bweni nchini Nigeria. Mkuu wa
Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya sambamba na kulaani mauaji hayo ametaka
magaidi waliofanya jinai hiyo kufuatiliwa kisheria. Bi Catherine Ashton
amesema, Umoja wa Ulaya unalaani mauaji ya wanafunzi 28 na mwalimu mmoja
huko Nigeria yaliyofanywa na kundi la Boko Haram na unaitaka serikali
ya Nigeria ihakikishe waliofanya jinai hiyo wanaadhibiwa kisheria.
Siku chache zilizopita, watu wenye silaha waliishambulia na kuichoma
moto shule moja kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuuwa wanafunzi 28
na mwalimu mmoja wa shule hiyo. Wakati huo huo, viongozi wa Nigeria
wametangaza kufungwa shule za sekondari katika jimbo la Yobe kufuatia
mauaji ya wanafunzi wa shule ya msingi yaliyofanywa siku ya Jumamosi.
No comments:
Post a Comment