Serikali ya Sudan na Chad kwa pamoja zimeamua kushirikiana kwa
minajili ya kuwatia mbaroni watu waliohusika wa mauaji ya Mkuu wa
Harakati ya Uadilifu na Usawa na msaidizi wake ndani ya mipaka ya ardhi
ya Chad.
Yassir Ahmad Muhammad, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Jinai ya
Darfur amesema kuwa, zoezi la kuwasaka watu waliohusika na jinai ya
kumuua Muhammad Bashar AbdulRahman mkuu wa harakati hiyo na msaidizi
wake limekwishaanza.
Amesema kuwa, hadi sasa idara ya upepelezi ya
Sudan inawatuhumu watu 18 kwa kuhusika na mauaji hayo na kusisitiza
kwamba, tukio hilo limepangwa kwa lengo la kuzusha ghasia na machafuko
zaidi katika jimbo la Darfur.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi uliopita Muhammad Bashar akiwa
pamoja na msaidizi wake waliuawa ndani ya mpaka wa Chad, shambulio
lililofanywa na waasi wanaofungamana na kundi la Uadilifu na Usawa tawi
la Jibril Ibrahim.
No comments:
Post a Comment