Duru za Pentagon zimeeleza kuwa, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck
Hagel aliwasiliana na mwenzake wa Misri Jenerali Abdul-Fattah al Sissi
mara mbili wiki iliyopita huku Misri ikiwa katika mgogoro.
Afisa wa habari wa Pentagon George Little amesema hayo na bila kutoa
maelezo zaidi, ingawa wengi wanaamini kuwa, kuna mkono wa Marekani
katika matukio yanayojiri nchini Misri. Hii ni katika hali ambayo baada
ya kupinduliwa Mursi, Rais Barack Obama wa Marekani amesema kwamba, ana
matumaini demokrasia itaimarishwa tena nchini Misri kwa kuchaguliwa
serikali mpya.
Saudi Arabia na Imarati zimekaribisha kuteuliwa Adly Mansour kuwa
kiongozi wa mpito wa Misri baada ya Mursi kung'olewa madarakani na
jeshi. Jeshi la Misri lilichukua uamuzi wa kumuondoa madarakani Rais
Muhammad Mursi baada ya maandamano makubwa ya kumpinga na baada ya kutoa
muda wa masaa 48 ya kutatuliwa mgogoro huo yaliyomalizika hapo jana.
Hata hivyo Musri amesema kupitia mtandao wake wa Facebook kuwa, anapinga
uamuzi huo wa jeshi aliouita kuwa ni mapinduzi ya kijeshi na amewataka
Wamisri kuheshimu katiba na sheria na kutoliunga mkono jeshi.
No comments:
Post a Comment